Pages

Saturday, May 18, 2013

Kuna Tofauti Kubwa kati ya kuimba wimbo wa sifa na Kusifu


Kuna Tofauti KUBWA SANA Kati Ya Kuimba WIMBO Wa Kusifu Na KuSIFU Kwenyewe… 

Kuimba Wimbo Wa KuSIFU Ni Tendo La Kufungua MDOMO Na Kutoa Sauti Ya Wimbo, Ila KUSIFU
Kwenyewe Ni Tendo La Kufungua MOYO Na Kutoa Sauti Ya Moyo Wako Mbele Za Mungu Ukielezea Sifa Zake, Yaani Vile Alivyo Na Atakavyokuwa Milele!


KuSIFU Si Zoezi La Sauti Na Mpangilio Wa Muziki Na Ubora Wa Utunzi.
KuSIFU Ni IBADA Ambapo SADAKA Ya Moyo Wa Mtu Hutolewa MADHABAHUNI Kwa Mungu Aliye Hai. Na Mungu Akiona Hilo Hushuka Pale KUIPOKEA…Na Kila Mahali Mungu Ashukapo, Lazima Litokee Badiliko; 
WAGONJWA HUPONYWA, 
MASIKINI HUTAJIRISHWA, 
WALIOCHOKA HUTIWA NGUVU, 
MATASA HUPATA UWEZO WA KUZAA TENA, 
WALIOFUNGWA HUFUNGULIWA TENA, 
WASIOOKOLEWA HUJA KWA YESU!
nk.

Kinachotokea Kwenye MADHEHEBU Na Dini Zetu Ni Kwamba KUSIFU Kumekuwa SEHEMU Ya Ibada Na Si IBADA Kamili. Hivyo Uhalisi, Nguvu Na Utukufu Wake Vimepungua!
NDIVYO ILIVYO HATA KWENYE IBADA YA KUABUDU, Inajitegemea Na Ina Thamani Kubwa Mbele Za Mungu Kuliko Watu Wanavyodhani. Ni Ibada Iliyojaa UDHIHIRISHO NA MTEMBEO WA ROHO MTAKATIFU Kama IKIPEWA HADHI YAKE!

SIFU kutoka MOYONI na Siokutoka MDOMONI

No comments:

Post a Comment